Msanii wa muziki kutoka Kenya, Toxic Lyrikali, ameendelea kuthibitisha ukuaji na ushawishi wake kimataifa baada ya kufichua orodha ya nchi sita zinazoongoza kwa kusikiliza muziki wake.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, Kenya inaongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kama taifa linalomsikiliza zaidi, ikifuatiwa na Jamaica katika nafasi ya pili. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Marekani, huku Trinidad and Tobago ikifuata katika nafasi ya nne.
India imejipatia nafasi ya tano kwenye orodha hiyo, huku Uingereza ikifunga orodha ya nchi sita zinazoongoza kwa kuupa muziki wa Toxic Lyrikali mapenzi makubwa.
Mafanikio hayo yanaonyesha jinsi muziki wa Toxic Lyrikali unavyoendelea kuvuka mipaka na kuwafikia mashabiki kutoka mataifa mbalimbali duniani, jambo linalothibitisha ukuaji wake kwenye soko la kimataifa.