Msanii na rapper Toxic Lyrikali amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu bifu inayodaiwa kuendelea kati ya vijana wa Nairobi West na Eastlands, akitaka tofauti hizo kukomeshwa na vijana waelekeze nguvu kwenye shughuli za kujijenga kimaisha.
Katika ujumbe wake kwa mashabiki kwenye moja ya show yake, Toxic Lyrikali ameweka wazi kuwa mvutano wa maeneo hautoi faida yoyote kwa vijana, na badala yake unawazuia kuona fursa muhimu zinazoweza kubadili maisha yao.
Mkali huyo wa ngoma ya Euphoria, amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kufikiria zaidi kuhusu kutafuta kipato, kubuni miradi na kujenga mustakabali imara badala ya kuendeleza bifu zisizo na tija.
Kauli yake imepokelewa kwa msisimko kwenye mitandao ya kijamii, ambapo wadau wa muziki na mashabiki wamempongeza kwa kuonyesha uongozi na kutoa wito wa umoja. Wengi wamesema kuwa ujumbe huo unawatia moyo vijana kuachana na tofauti za maeneo ambazo mara nyingi huibua migogoro ya kijamii.