
Msanii wa Hip Hop nchini Kenya, Toxic Lyrikali, ameibua gumzo mtandaoni baada ya kuwajibu vikali wakosoaji wanaodai kuwa ana kiburi. Kupitia mitandao ya kijamii, msanii huyo alionekana kukerwa na lawama hizo, akisema kuwa watu wanaomuita mkiburi hawafahamu muktadha wa ujumbe wake.
“Wenye wanasema niko na kiburi wanaskizanga bongo,” Toxic aliandika.
Kauli hiyo imewagawa mashabiki wake, huku baadhi wakimtetea wakisema anazungumza kwa uhalisia, na wengine wakimshutumu kwa majivuno na dharau kwa wasanii wachanga.
Kauli hii imekuja siku mbili tu baada ya msanii huyo kuwashauri wasanii chipukizi kutomlipa pesa kwa ajili ya kufanya collabo naye, bali waitumie hiyo hela kujiendeleza kimuziki
“Pesa unataka kunipea ya collabo, fanya nayo do ba deadly,” aliandika instagram.
Kauli hizi zimezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea kwa kusema anazungumza ukweli mgumu ambao wengi wanaogopa kusema, huku wengine wakimshutumu kwa majivuno na kuwakandamiza wasanii wachanga.