
Rapper Travis Scott ametajwa kuwa msanii Kinara katika tamasha la Day N Vegas ambalo litafanyika September 2 hadi 4 Jijini Las Vegas nchini Marekani.
Hili linakuwa tamasha lake la kwanza nchini Marekani tangu Janga lililotokea kwenye tamasha lake la ‘Astroworld Festival’ mwaka 2021 na kuchukua maisha ya watu 10 na namba kubwa ya majeruhi.
Travis Scott alikuwa ‘booked’ kutumbuiza katika tamasha la Day N Vegas mwaka Jana lakini waandaaji wa tamasha hilo ilibidi wamuondoe kwenye orodha kufuatia Janga hilo ambalo lililotokea kwenye tamasha lake wiki chache nyuma na kuteka hisia za watu wengi nchini Marekani.