Gossip

Trevor: Mungai Eve Anapaswa Kuomba Radhi Kwa Mashabiki

Trevor: Mungai Eve Anapaswa Kuomba Radhi Kwa Mashabiki

Aliyekuwa mpenzi na mshirika wa karibu wa kibiashara wa Mungai Eve, Director Trevor, ameweka wazi mtazamo wake kuhusu sakata linalomkumba mrembo huyo baada ya kutoa kauli tata katika mahojiano akidai kwamba hawezi toka kimapenzi na mwanaume mwenye kipato cha chini.

Kwa mujibu wa Trevor, tamko hilo limekuwa na athari kubwa kwa taswira ya Mungai Eve na limepelekea mashabiki wengi kujitenga naye, wakieleza kuwa maneno yake ni kielelezo cha dharau kwa vijana wanaojitahidi kujikimu kwa kipato cha chini. Anasema maneno hayo yamejenga dhana ya kiburi na yamevunja uhusiano wa karibu aliokuwa nao na wafuasi waliomsaidia kufanikisha safari yake ya umaarufu.

Aidha, Trevor amesisitiza kuwa hatua ya kuomba radhi inaweza kuwa njia pekee ya kurejesha imani ya mashabiki na kupunguza ukosoaji unaoendelea kumwandama mrembo huyo ambaye juzi kati alikiri kupitia matatizo ya afya ya akili hasa baada ya kujutia maamuzi ya kumkimbia mwanaume ambaye alimpambania hadi kupata umaarufu mkubwa nchini Kenya.

Ikumbukwe katika mahojiano na Liz Jackson, Mungai Eve alinukuliwa akisema kuwa hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ambaye kipato chake kiko chini ya shilingi laki tano kwa mwezi. Kauli hiyo ilizua tafsiri kwamba anajiona bora kuliko watu wa kawaida, hali ambayo iliwakasirisha mashabiki na kuibua upinzani mkali dhidi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *