Entertainment

Trey Songz ajisalimisha kwa polisi New York

Trey Songz ajisalimisha kwa polisi New York

Nyota wa R&B kutoka Marekani Trey Songz amejikabidhi mwenyewe mikononi mwa polisi wa mjini New York kwa ajili ya kukabiliana na madai ya kuwapiga watu wawili.

Ripoti za awali zinasema kwamba Trey Songz alitembeza kipigo kwa mwanamke mmoja huku akimburuza kwa kuvuta nywele zake huko mjini new york, marekani lakini sasa mamlaka zinadai kwamba kulikuwa na mhanga mwingine ambaye alifikiwa na ngumi ya mwimbaji huyo na hivyo kuwa wawili.

Hivyo Trey Songz ametakiwa kwenda kusimama kizimbani kwenye mahakama kufuatia madai hayo. Mwanasheria wake aitwaye “mitch schuster” ameweka kifua mbele kwa kusema kwamba yeye yupo tayari kwa lolote lile.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *