
Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Trey Songz anazidi kuandamwa na tuhuma za ubakaji pamoja na unyanyasaji wa kingono, mwanamke wa tatu amejitokeza na kudai fidia ya shilling billion 2.3 za Kenya kwa madai ya kubakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile.
Kwa mujibu wa TMZ, shauri hilo lilifunguliwa Februari 15 mwaka huu ambapo mwanamke huyo alisema Trey Songz alimwalika kwenye party katika nyumba moja mjini Los Angeles, baadaye alimpeleka chumbani wakiwa na makubaliano ya kufanya mapenzi kawaida.
Walipofika chumbani, Trey Songz alimsukuma chini na kuanza kumlazimisha kumuingilia kinyume na maumbile, baada ya kupambana kujioka kwenye mikono ya mkali huyo wa R&B, mwanamke huyo anasema alizidiwa nguvu na Trey songz na hivyo akamuingilia kinyume na maumbile kwa nguvu.