
Msanii Trio Mio amewajibu mashabiki zake ambao wanatilia shaka uwezo wake wa kuachia nyimbo kali baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha nne.
Kwenye mahojiano na Vicent Mboya amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwa kuwa shule ndio ilikuwa kizingiti kwenye suala la kuachia nyimbo mfululizo, hivyo anaamini kuwa kukamilisha kwake masomo kutamsaidia kuelekeza nguvu zake kuboresha muziki wake.
Kauli yake imekuja baada ya walimwengu kuhoji kuwa huenda akakumbana na mambo yatakayomzuia kuendelea na muziki wake ikiwemo mahusiano ya kimapenzi na wanawake tofauti.