
Rapa anayekuja kwa kasi nchini Trio Mio amechukua mapumziko mafupi kwenye muziki wake kwa ajili ya kujiandaa kukalia mtihani wake wa kitaifa wa kidato cha nne.
Rapa huyo amethibitisha hilo kupita ukurasa wake wa twitter ambapo ametoa angalizo kwa wanamuziki wenzake kujipanga kisanaa la sivyo akirejea mwakani atawaonyesha kivumbi kwenye tasnia ya muziki.
Hata hivyo kauli yake imezua hisia mseto miongoni mwa wakenya ambapo wengi wamemtaka rapa huyo aache majigambo na badala ya kuelekeza nguvu zake kwenye matayarisho ya mtihani wa kidato cha nne
Utakumbuka Trio Mio ambaye ana umri wa miaka 18 alipata umaarufu nchini kipindi cha corona kupitia wimbo wake uitwao Cheza Kama Wewe na tangu kipindi hicho amekuwa akiachia nyimbo mfululizo bila kupoa kiasi cha watu kuanza kumfananisha na Marehemu E-Sir, moja kati ya marapa walioacha alama kwenye muziki wa kizazi kipya nchini Kenya.