Entertainment

TUHUMA ZA MAUJI ZAZIDI KUMUANDAMA SPICE DIANA

TUHUMA ZA MAUJI ZAZIDI KUMUANDAMA SPICE DIANA

Sakata la kijana aliyewauwa nyumbani kwa Spice Diana Henry Nsamba limechukua sura mpya baada ya Mulindwa Lawrence ambaye ni kaka wa mwendazake kudai kuwa ndugu yake alikuwa ana mpango wa kufanya wimbo wa pamoja na msanii huyo.

Kulingana na Lawrence, Nsamba alikuwa anafanya vibarua ya kutengeneza matofali mitaani kwa ajili ya kuchangisha pesa za kufanikisha kolabo yake na spice diana kwa sababu alikuwa na ndoto ya kuwa mwiimbaji lakini kwa masikitiko makubwa akakutana na mauti yake.

Aidha amedai kuwa Spice Diana na meneja wake Roger Lubega walikula pesa za ndugu yake na waliposhindwa kumrejeshea haki yake wakaamua kumwekelea madai ya wizi ambayo yalimpelekea kupigwa hadi kufa nyumbani kwa msanii huyo.

β€œThey are using theft to hide the truth. Nsamba was not capable of robbery. He wanted to collaborate with Spice Diana hence frequenting her residence. He paid Roger Lubega and Spice Diana for the collaboration. They thumped him for demanding it,” amesema Mulindwa Lawrence kaka wa mwendazake Henry Nsamba.

Hata hivyo Spice Diana na uongozi wake wamesalia juu ya tuhuma ya mauji ya kijana huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *