Entertainment

Tuzo za iHeartRadio zaongeza kipengele kipya cha msanii bora wa Afrobeats

Tuzo za iHeartRadio zaongeza kipengele kipya cha msanii bora wa Afrobeats

Kituo cha iHeartRadio kimeanika wazi vipengele vya Tuzo zake za Muziki ambapo kwa mwaka huu kuna kipengele kipya kimeongezwa, ni Afrobeats Artist of the Year.

Kwenye kipengele hicho kipya, wakali kutoka nchini Nigeria; Burna Boy, CKay, Tems, Wizkid na Fireboy DML wametajwa kuchuana.

Ni kama tu ni marudio ya Soul Train Awards 2022, ambapo wasanii hao hao watano walitajwa kwenye vipengele tofauti tofauti vya tuzo hizo kubwa zinazotolewa na kituo cha Televisheni cha BET.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *