Entertainment

Upendo Nkone Atoa Wito wa Tumaini na Msamaha Kuelekea Mwaka Mpya 2026

Upendo Nkone Atoa Wito wa Tumaini na Msamaha Kuelekea Mwaka Mpya 2026

Msanii wa muziki wa Injili, Upendo Nkone, amewahamasisha mashabiki na waumini kuhitimisha mwaka kwa furaha, amani na uchangamfu, akisisitiza umuhimu wa kujisamehe na kuanza upya bila lawama.

Katika ujumbe wake wa mwisho wa mwaka, Upendo amewataka watu wajisamehe kwa makosa waliyofanya wao wenyewe pamoja na malengo ambayo hawakuweza kuyatimiza katika mwaka unaoisha wa 2025. Amesisitiza kuwa badala ya kujilaumu, ni muhimu kujipanga upya na kuelekeza nguvu kwenye mwanzo mpya wenye matumaini.

Msanii huyo wa Injili pia amegusia suala la msamaha kwa wengine, akiwahimiza watu kuwasamehe waliowakosea hata pale ambapo wahusika hao wanaonekana kutotambua au kujali makosa yao.

Upendo Nkone amehitimisha kwa kuwakumbusha mashabiki na waumini kuanza mwaka mpya wakiwa na Yesu Kristo, akieleza kuwa kumweka Kristo mbele ni njia ya kupata msaada, mwelekeo na nguvu mpya katika safari ya maisha. Ameonyesha pia upendo wake kwa mashabiki wake kwa kuwatakia baraka na heri wanapoelekea mwaka mpya 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *