
Kinara wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amewataka mashabiki wake kuwakimbia wasanii wasiounga mkono chama chake cha kisiasa.
Kwenye video iliyodakwa na tovuti moja ya habari nchini Uganda, Bobi Wine amesikika akiwataka wafuasi wake kutohudhuria matamasha ya watu wanaowaunga mkono mpinzani wake.
“Tafadhali msijihusishe na wale wanaotupinga, msiwaunge mkono kwa namna yoyote kwa sababu ni sehemu ya wakandamizaji wetu. Hatuwezi kuwa marafiki nao wakati wanakutumia kuwakandamiza watu wangu,” alisema.
Bobi Wine amehoji kuwa mashabiki kindakindaki wa chama hicho huwa wanaunga mkono shughuli za wanamuziki wanaonesha utii kwa chama cha NUP.
“Lakini kwa upande mwingine unapaswa kuwasaidia wale wote wanaotumia sauti na talanta zao kupambana na dhuluma,” aliongeza.