
Staa wa muziki wa Bongofleva, Vanessa Mdee amesema alipatwa na msongo wa mawazo baada ya kujifungua mtoto wake kwanza, Seven.
Kwenye mahojiano na Podcast ya Swahili Nation Vanessa amesema msongo wa mawazo baada ya kujifungua ulimletea madhara licha ya sapoti kubwa anayopata kutoka mchumba wake, Rotimi.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Bambino” amesema kuwa watu wengi hawaelewi huzuni hiyo na labda wanapomwona mtandaoni akiwa na furaha hudhania kuwa ana furaha maishani mwake.
Hata hivyo amewataka wanaume na hata kila mtu katika Jamii kukomesha unyanyapaa dhidi ya afya ya akili kwani kwa sasa anajaribu kupona na ana matumaini mambo yatakuwa sawa.