 
									Socialite kutoka Kenya, Vera Sidika, amefichua kuwa hununua simu zake za iPhone moja kwa moja kutoka maduka rasmi ya Apple nchini Marekani na siyo Kenya kama namna baadhi ya watu wanavyodai.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Vera amesema kuwa hana imani na maduka mengi yanayouza vifaa vya teknolojia nchini humo, akieleza kuwa baadhi ya simu hizo huwa hazitoki moja kwa moja kwa Apple na huwa zimefanyiwa marekebisho kabla ya kuuzwa.
Mama huyo wa watoto wawili, amesema hatua hiyo ni njia yake ya kujihakikishia ubora na usalama wa kifaa anachonunua, ikizingatiwa kwamba bidhaa ghushi zimekuwa changamoto kubwa sokoni.
Kauli yake imezua mjadala mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimuunga mkono kwa kusema kuwa bidhaa bandia zimekuwa changamoto kubwa sokoni, huku wengine wakidai kuwa anajaribu kuonesha maisha ya kifahari.
 
								 
             
             
                             
                             
                             
                             
                             
                             
                            