LifeStyle

Vera Sidika Ajibu Madai ya Kuwatelekeza Watoto Wake

Vera Sidika Ajibu Madai ya Kuwatelekeza Watoto Wake

Socialite maarufu nchini Kenya, Vera Sidika, amejibu tetesi kutoka kwa mashabiki waliodai kwamba amewatelekeza watoto wake kwa sababu ya kuwa safarini mara kwa mara.

Kupitia ujumbe alioweka mtandaoni, Vera amesisitiza kuwa watoto wake daima wako chini ya uangalizi wa mzazi kila wakati. Amefafanua kuwa anapohitajika kuwa kwenye shughuli zake binafsi au kuendesha mikusanyiko katika nyumba yake ya kifahari, huomba baba ya watoto wake Brown Mauzo kukaa nao muda wote.

Aidha,Mwanamama huyo amesema anaposafiri kwenda maeneo mbalimbali duniani, baba ya watoto hubaki nao nyumbani akisaidiana na wafanyikazi wa ndani (nannies) hadi atakaporudi.

Kauli hiyo imekuja baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuibua maswali kuhusu malezi ya watoto wake, baadhi ya watu wakimlaumu kwa kutokuwa karibu nao kutokana na ratiba zake za mara kwa mara za safari na shughuli za kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *