Gossip

Vera Sidika Amkana Brown Mauzo Kuhusu Simu za Usiku

Vera Sidika Amkana Brown Mauzo Kuhusu Simu za Usiku

Mrembo maarufu nchini Kenya Vera Sidika amemtolea uvivu mzazi mwenzake Brown Mauzo mitandaoni, baada ya mwanamuziki huyo kulalamikia simu za usiku wa manane.

Kupitia akaunti yake ya mitandao ya kijamii, Mrembo huyo amesema hajawahi kumpigia Mauzo akiwa mlevi wala kuanzisha drama, akimtaka aache kutumia jina lake kwa kiki.

Aidha, Vera ametishia kumuanika Mauzo kwa madai ya uongo, akidai hajawahi kugharamia mahitaji ya watoto wao tangu walipotengana.

Kauli yake imekuja baada ya mashabiki kumkosoa vikali wakidai kwamba anampigia mzazi mwenzie, Brown Mauzo, simu nyakati za usiku akiwa mlevi licha ya wawili hao kuachana rasmi. Baadhi ya wafuasi walionya kwamba kitendo hicho cha kumsumbua Mauzo huenda kikaathiri ndoa ya sasa ya msanii huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *