
Sosholaiti na mfanyabiashara maarufu Vera Sidika amevunja kimya kufuatia kejeli za mitandaoni kutoka kwa baadhi ya Wakenya waliomkejeli kwa kufanya club appearance mjini Busia, hatua ambayo baadhi waliiita “recession indicator” ya maisha yake.
Kupitia InstaStory yake, Vera alionekana kutoyumbishwa na maoni hayo, akisisitiza kuwa anajivunia kuwa na uwezo wa kuungana na mashabiki wake kote nchini, siyo tu katika miji mikubwa.
“Seems like Kenyans have just discovered a new vocabulary ‘Recession indicator’. Kwani what’s wrong with me making a club appearance in Busia?” aliandika Vera.
Katika ujumbe wake, Vera alifafanua kuwa hana aibu kufanya maonyesho au kujitokeza katika maeneo yote ya Kenya, kwani kila mahali kuna mashabiki wanaomheshimu na kumpenda.
“I love connecting with my fans in all parts of the country. Kama Busia wananitaka, basi nitaenda si kila mtu anaishi Nairobi!,” alisema.
Baadhi ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii waliiunga mkono kauli ya Vera, wakisema ni jambo la heshima kuonyesha usawa kwa mashabiki wote, bila ubaguzi wa kijiografia. Lakini kwa upande mwingine, baadhi walionekana kudharau tukio hilo, wakilitafsiri kama ishara ya kuporomoka kwa hadhi ya Vera kama staa wa muda mrefu.