Gossip

VERA SIDIKA AWAPA SOMO MABINTI WANAOTOKA KIMAPENZI NA MASPONSA

VERA SIDIKA AWAPA SOMO MABINTI WANAOTOKA KIMAPENZI NA MASPONSA

Mwanasosholaiti maarufu nchini Kenya, Vera Sidika ameshauri kina dada kuchukua fedha za Sponsa na kuwekeza.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, mmoja wa mashabiki wake alimuuliza ushauri wake kwa wasichana ambao wanatoka na watu wazima.

“Ushauri wako kwa msichana anayechumbia wababa,” Shabiki aliuliza.

“Kula pesa yake mzuri, lakini cha muhimu wekeza,”Alijibu Vera.

Utakumbuka Vera alipata umaarufu nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla mara baada ya kutokea kwenye video ya kundi la P Unit, You Guy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *