LifeStyle

Vera Sidika Azima Uvumi wa Mpenzi Kupiga Picha Zake

Vera Sidika Azima Uvumi wa Mpenzi Kupiga Picha Zake

Socialite maarufu Vera Sidika amewaacha mashabiki wake wakiwa na mshangao baada ya kufichua kuwa yeye husafiri peke yake na hupiga picha zake zote mwenyewe akitumia remote ndogo na standi ya simu.

Kupitia Instastory zake, Vera ameonyesha kifaa kidogo cha remote anachotumia kupiga picha, akieleza kuwa kama msafiri wa pekee yake, hupendelea njia hiyo badala ya kuwaomba watu wasiofahamika kumpiga picha.

Mwanamama huyo amesema kuwa mara nyingi unapomuomba mgeni akupige picha, matokeo huwa si mazuri, hivyo amejizoesha kutumia teknolojia hiyo ndogo kumsaidia kupata picha anazotaka kwa urahisi.

Kauli yake imekuja baada ya mashabiki wengi kuuliza mara kwa mara ni nani anayempiga picha anapokuwa safarini, kwani picha zake zimekuwa zikionekana za kitaalamu na zenye ubora wa juu.

Baadhi ya mashabiki walidhani picha hizo zilikuwa zikichukuliwa na mpenzi wake, lakini Vera aamepuzilia mbali uvumi huo kwa kueleza wazi kuwa hana mpenzi kwa sasa na anaishi maisha ya ujasiri kama mwanamke anayejitegemea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *