Gossip

Vera Sidika: Nimechoka Kuwa Single, Nataka Mchumba Gen Z

Vera Sidika: Nimechoka Kuwa Single, Nataka Mchumba Gen Z

Socialite maarufu wa Kenya, Vera Sidika, amefichua kuwa sasa yuko tayari kurudi tena kwenye ulimwengu wa mapenzi na safari hii, anavutiwa na mwanaume wa kizazi cha Gen Z.

Vera, ambaye ni mama wa watoto wawili, amekiri kuwa amekuwa single kwa muda mrefu sana na amekuwa akipitia kipindi kigumu cha upweke, akisema hata siku yake ya kuzaliwa mwaka huu haikuwa na msisimko kama ilivyokuwa zamani.

Amesema hali hiyo imemfanya atambue umuhimu wa kuwa na mtu wa karibu, na sasa anaona yuko tayari kufungua moyo wake tena kwa mapenzi.

Vera ameeleza kuwa anavutiwa na wanaume wa Gen Z kwa sababu wanajua kuonyesha mapenzi kwa vitendo, na hawana hofu ya kuzungumza hisia zao. Pia amesema vijana hao wana nguvu na hulka ya furaha, jambo analoamini litampa msisimko mpya maishani.

Kauli yake imezua maoni mseto mtandaoni, baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa ujasiri wa kusema ukweli wake, huku wengine wakimtania kwa kutaka mwanaume kijana zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *