Gossip

Video ya Khaligraph na Toxic Lyrikali Yazidisha Uvumi wa Kolabo, 

Video ya Khaligraph na Toxic Lyrikali Yazidisha Uvumi wa Kolabo, 

Rapa kutoka Kenya, Khaligraph Jones, amewaacha mashabiki na maswali baada ya kuonekana akizungumza na msanii Toxic Lyrikali wakati wa mazoezi ya Sol Fest. Tukio hilo lilinaswa kwenye video na kusambaa haraka mitandaoni, likichochea uvumi kuwa huenda wawili hao wanapanga kufanya kazi pamoja.

Kwenye klipu hiyo, wasanii hao wanaonekana wakisalimiana nyuma ya jukwaa, jambo lililowafanya mashabiki kudhani kuwa huenda kuna mipango mipya ya muziki inayonukia.

Hii inakuja licha ya kwamba Toxic Lyrikali aliwahi kukataa ombi la kolabo kutoka kwa Khaligraph hapo awali, akieleza kuwa wakati huo haukuwa sahihi. Hata hivyo, kukutana kwao ghafla katika mazoezi ya Sol Fest kumezua matumaini mapya kuwa msimamo huo huenda umebadilika.

Ingawa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa yeyote kati yao, mashabiki wanaendelea kuonyesha matumaini makubwa kwamba kukutana kwao unaweza kuwa mwanzo wa kolabo inayosubiriwa kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *