
Video ya wimbo wa Killy ‘Ni Wewe’ ambao amemshirikisha Harmoninze imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na malalamiko ya hakimiliki.
Kwa sasa video hiyo haipatikani kwenye mtandao huo kufuatia malalamiko ya hakimiliki kutoka kwa Mutisya Munyithya.
“This video is no longer available due to a copyrighty claims by Ian Mutisya Munyithya” taarifa ya YouTube inaeleza.
Mdundo wa wimbo wa ni wewe wake killy inafanana kwa kiasi kikubwa na wa wimbo maarufu wa zamani kundi la muziki la Les Wanyika, Sina makosa.
Ikumbukwe mtandao wa Youtube hauruhusu kutumia kazi au kionjo cha mtu mwengine bila makubaliano.