Entertainment

Vindee Aomba Radhi Baada ya Kudai Ana Ukaribu na IShowSpeed

Vindee Aomba Radhi Baada ya Kudai Ana Ukaribu na IShowSpeed

Prankster kutoka Kenya Vindee ameomba radhi Wakenya baada ya kudai awali kuwa alikuwa katika mawasiliano na staa wa mitandao ya kijamii, IShowSpeed, kuhusiana na ziara yake nchini humo.

Kupitia taarifa rasmi aliyotoa mtandaoni, Vindee amesema lengo lake halikuwa kuwapotosha watu wala kutafuta kiki, akisisitiza kuwa ni mzaha uliotoka nje ya muktadha uliokusudiwa.

Ameongeza kuwa licha ya watu mbalimbali kumshawishi na hata kujaribu kumuonga kwa maelfu ya pesa, alikataa kabisa kwa kuwa alihofia hatua hiyo ingemletea matatizo makubwa baadaye.

Vindee amesema amejifunza kutokana na tukio hilo na kuahidi kuwa makini zaidi na maudhui anayotoa kwa umma, akitoa wito kwa mashabiki na umma kwa ujumla wasimchukulie vibaya.

Kauli ya Vindee imekuja muda mfupi baada ya video yake kusambaa mitandaoni, ikimuonyesha akishindwa hata kumsalimia IShowSpeed walipokutana ana kwa ana, hali iliyozua maswali mengi kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakiamini kuwa wawili hao walikuwa wakizungumza mara kwa mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *