
Female singer kutoka Uganda Vinka amekanusha madai ya kuwakodisha walinzi kwa ajili ya kumpa usalama wakati wa shows zake.
Kupitia ukurasa wake wa twitter vinka amesema kuwa wanaume wawili ambao huandamana nao kwenye shows zake sio walinzi wake bali ni timu inayounda menejiment yake.
Hitmaker huyo wa “Thank God” amewataka wanablogu nchini Uganda kukoma kueneza taarifa za uongo kuwa amekodisha mabouncers kwa ajili ya kumpa walinzi.
Kauli ya Vinka imekuja mara baada ya kurasa moja ya udaku kuikejeli picha yake kwenye mtandao wa twitter kwa kusema kwamba mmoja wa walinzi wa vinka anahitaji usalama kutokana na kuwa na mwili mdogo.