Entertainment

VIVIAN AICHANA KAMPUNI YA NGOMMA KWA KUPORA MIRABAHA YA NYIMBO ZAKE

VIVIAN AICHANA KAMPUNI YA NGOMMA KWA KUPORA MIRABAHA YA NYIMBO ZAKE

Female singer kutoka Kenya Vivian ameamua kuichana Kampuni inayoongoza katika kusambaza muziki na kukusanya mirabaha ya wasanii huru, Ngomma,  kwa kile anachodai kwamba haijamlipa pesa zake zilizotokana na muziki wake kuuzwa.

Kupitia waraka mrefu aliouandika kwenye mtandao wa Instagram Vivian amesema hajalipwa na hafahamu ni kiasi gani cha pesa Kampuni ya Ngomma imeingiza kutoka kwenye muziki wake.

Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kuitaka kampuni Ngomma impe hakimiliki ya nyimbo zake zote ambazo amezitolea jasho huku akitishia kuichukulia kampuni hiyo hatua kali za kisheria ili dunia ione udhalimu wake.

Hata hivyo amewataka mashabiki wawe na subira kipindi hiki anapambania hakimiliki za nyimbo zake kwani anakuja na kitu kipya kwa ajili yao.

Ikumbukwe katika siku za hivi karibuni wasanii wa humu nchini wamekuwa wakizisuta vikali bodi zilizopewa jukumu la kukusanya pesa za wasanii nchini huku wakitaka bodi hizo zuchunguzwe ili wasanii wapate haki yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *