Entertainment

Wachambuzi Wabashiri GNX ya Kendrick Kushinda Album Bora ya Mwaka

Wachambuzi Wabashiri GNX ya Kendrick Kushinda Album Bora ya Mwaka

Wachambuzi wa muziki duniani wanaitabiria album mpya ya Kendrick Lamar, GNX, kushinda tuzo ya Album Bora ya Mwaka kwenye Grammy 2026. Ikiwa atashinda, Kendrick atavunja rekodi ya kuwa msanii wa rap (Solo) wa kwanza kushinda kipengele hicho.

Ushindi wa GNX utaimarisha nafasi yake kama mmoja wa wasanii wa hip-hop wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, huku akikaribia kuvunja rekodi ya Jay Z na Kanye West kwa kushinda Grammy nyingi zaidi kwa rapper.

Baadhi ya hit songs kutoka kwenye album hiyo zimechochea imani kuwa GNX ni bora. Kwa ujumla, GNX ni album iliyojaa uandishi wa hali ya juu, inafanya vizuri kwenye mauzo ndiyo maana wengi wanaamini, Grammy 2026 itashinda kipengele cha Album bora.