Entertainment

Wakadinali Watawala Unkut Hip Hop Awards 2025 Kwa Ushindi Mkubwa

Wakadinali Watawala Unkut Hip Hop Awards 2025 Kwa Ushindi Mkubwa

Kikundi cha hip-hop Wakadinali kimetawala tuzo za Unkut Hip Hop Awards 2025, baada ya kuibuka na ushindi katika vipengele vitatu vikubwa

Wakadinali walinyakua tuzo ya Album of the Year, ushindi unaokuja kutokana na mapokezi ya Victims of Madness 2.0, Albamu ambayo umesifiwa kwa ubora wa uzalishaji, ubunifu wa ala, na ukomavu wa maudhui.

Mwanachama wa kundi hilo, Scar Mkadinali, alitangazwa Lyricist of the Year, akitambuliwa kwa ustadi wake wa uandishi, weledi katika vina, na uwezo wa kuwasilisha simulizi zenye uzito na uchambuzi wa kijamii.

Kundi zima la Wakadinali pia lilitunukiwa tuzo ya Group of the Year, likidhibitisha kuwa wanachukua nafasi kuu katika kuiongoza hip-hop ya Kenya kupitia kazi thabiti na ushawishi wao mkubwa kwenye mitandao na mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *