Bifu kati ya Wakuu Music, na rapa Toxic, limechukua sura mpya baada ya Wakuu kuachia diss track yao ya pili iitwayo “Coffin,” ambayo inamlenga moja kwa moja msanii Toxic Lyrikali.
Hii inakuja siku chache tu baada ya Toxic Lyrikali kupuzilia mbali diss track ya kwanza kwa kuita mchongoana ambapo alienda mbali zaidi na kusema kwamba hana muda wa kujibizana na wasanii wanaotafuta umaarufu kupitia mafanikio yake ya muziki.
Katika diss track ya “Coffin,” Wakuu Music amejibu kwa toni kali zaidi, akichana kwa maneno makali na mafumbo yanayoashiria kuongezeka kwa mvutano kati yao na mpinzani wao. Diss track hiyo imeibua hisia kali mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakisifu ubunifu na uchezaji wa maneno, huku wengine wakisema bifu hiyo inazidi kupandisha joto la ushindani katika muziki wa Hiphop.
Mashabiki sasa wanasubiri kuona kama Toxic Lyrikali atajibu au ataendelea kupuuzia kama alivyofanya kwa diss track ya kwanza.