
Walimwengu mtandaoni wamewatolea uvivu staa wa muziki nchini Willy Paul baada msanii huyo kudai kuna binti wa mwigizaji wa kipindi cha Vioja Mahakama amemuibia simu aina iPhone nyumbani kwake.
Kupitia comments walizoziachia katika post ya Willy Paul kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram wamemtaka msanii huyo aache suala la kuendekeza kiki kwenye muziki wake na badala yake atoe muziki mzuri ambao utajiuza wenyewe.
Aidha wameenda mbali zaidi na kusema kwamba hitmaker huyo wa ngoma ya “Toto” amekosa ubunifu kwenye masuala ya kutengeneza matukio yatakayomfanya azungumziwe mtandaoni kwani kiki aliyoitengeneza haina mashiko ya kuteka hisia za watu.
Kauli hiyo ya walimwengu imekuja mara baada ya Willy Paul kumpa binti anayedai kuwa ni wa mwigizaji wa Vioja Mahakama makataa ya siku moja kurejesha simu yake la sivyo atamuaibisha vibaya baba yake mzazi.