
Wasanii wa Nigeria wanaendelea kuwafundisha kazi wasanii wa mataifa mengine barani Afrika, waitawala Tracklist ya Soundtracks za filamu ya “Black Panther: Wakanda Forever” yenye Jumla ya nyimbo 19.
Mbali na Rihanna, wasanii wa Nigeria wameshiriki kwa ukubwa kwenye Soundtrack ya filamu hiyo akiwemo Burna Boy, Tems, Fireboy DML, CKay na Rema. Album hiyo imetayarishwa na Ryan Coogler, Ludwig Göransson, Archie Davis na Dave Jordan.
Göransson ametumia zaidi ya masaa 2500 akirekodi Soundtrack hizo kwenye studio 6 tofauti, kwenye mabara matatu na mataifa Matano. Mashabiki watapata kusikia sauti za wasanii zaidi ya 250 kwenye filamu hiyo ambayo imetajwa kuachiwa rasmi Novemba 11 mwaka huu.