Entertainment

Wasanii wa Tanzania Wapata Hasara Kubwa Baada ya Maandamano

Wasanii wa Tanzania Wapata Hasara Kubwa Baada ya Maandamano

Maandamano makubwa yaliyolenga kupinga kile kinachoelezwa kuwa udhalimu wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, yamegeuka kuwa janga kwa baadhi ya wasanii wa Bongofleva, baada ya biashara zao kuripotiwa kushambuliwa, kuvunjwa na kuchomwa moto na waandamanaji wenye hasira.

Jijini Dar es Salaam, mgahawa maarufu wa Shishi Food, unaomilikiwa na msanii wa muziki Shilole, umeungua moto vibaya usiku wa kuamkia leo. Tukio hilo linadaiwa kufanywa na kundi la waandamanaji waliokuwa wakilenga biashara na mali zinazohusishwa na mastaa wanaoonekana kuunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Shilole, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akionyesha uhusiano wa karibu na serikali, amekumbwa na hasara kubwa kutokana na tukio hilo. Mashuhuda wanasema moto ulianza ghafla baada ya kundi la vijana kuvamia mgahawa huo, wakipiga kelele za kuipinga serikali.

Hasara hiyo pia imewapata wasanii wengine akiwemo Billnass, ambaye duka lake limechomwa moto, na Jux, ambaye duka lake limevunjwa na kuporwa mali ikiwemo nguo na vifaa vya thamani. Wakati huo huo, Makjuice Sinza, biashara inayomilikiwa na watu wa karibu na tasnia ya burudani, imeripotiwa kuharibiwa na kuporwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *