Gossip

Weasel Afichua Sababu ya Kuachana na Sugar Mamas

Weasel Afichua Sababu ya Kuachana na Sugar Mamas

Mwanamuziki maarufu Weasel amefichua wazi kuwa licha ya kuwa na historia ndefu ya uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi, hataki tena kuhusishwa na wanawake wakubwa kiumri wenye pesa maarufu kama sugar mamas.

Katika mahojiano ya hivi karibuni, msanii huyo alikiri kuwa aliwahi kuchumbiana na city cougars kwa kipindi fulani, lakini sasa ameamua kuachana kabisa nao kwa kile alichokitaja kuwa ni uhusiano usio na tija.

“Sikuwahi kufaidika chochote cha maana kutoka kwa mahusiano niliyokuwa nayo na sugar mamas. Ni kupoteza muda tu. Hawachangii maendeleo yoyote ya kweli kama watu wanavyodhani,” alisema Weasel.

Msanii huyo kutoka Uganda alisisitiza kuwa sasa ameamua kumakinika kwenye familia yake, hasa mahusiano yake na mama wa watoto wake, Sandra Teta, ambaye kwa sasa ndiye kipenzi chake pekee.

“Niliwahi kutoka na sugar mamas, lakini niliwacha. Sasa akili yangu yote iko kwa Sandra na watoto wetu. Hapo ndipo moyo wangu uko,” aliongeza.

Weasel pia aliwaonya wasanii wenzake dhidi ya kuvutiwa na maisha ya mapenzi na sugar mamas, akiwashauri wawe na malengo ya muda mrefu na kuweka bidii katika kazi zao.

“Wasanii wengi hupotea njia kwa sababu ya tamaa. Badala ya kujijenga kwenye muziki, wanajikuta wamelala na wanawake wenye umri mkubwa wanaowapotezea muda,” alionya.

Kauli ya Weasel imepokewa kwa hisia tofauti mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa hatua hiyo ya kimaamuzi, huku wengine wakimshangaa kutokana na historia yake ya mapenzi yenye utata. Hata hivyo, Weasel anaonekana kuwa katika njia mpya ya maisha, akiwa na mtazamo wa kutulia na kuzingatia familia na kazi.