
Mwanamuziki kutoka Uganda Douglas Mayanja maarufu kama Weasel Manizo kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya kile kilichotokea kati yake na mfanyikazi wake wa nyumbani ambaye aliripotiwa kupigwa na msanii huyo.
Akiwa kwenye moja ya Interview, Weasel amekanusha kumshushia kichapo mfanyikazi wake wa nyumbani huku akisema kwamba alisikia uvumi huo kutoka kwa vyombo vya habari na majukwaa mengine.
Hitmaker huyo wa “Magnetic” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa vyombo vya habari vilirusha taarifa hiyo bila kujua kiini cha kupigwa kwa mfanyikazi wake wa nyumbani.
Hata hivyo amesema licha ya mfanyikazi wake wa nyumbani kueleza upande wake wa stori,anasubiri apate nafuu ili aweze kuweka wazi kilichotokea kati yao kwa kina.