Entertainment

WEASEL MANIZO AWAJIBU WANAOTAKA AACHIE NYIMBO MPYA

WEASEL MANIZO AWAJIBU WANAOTAKA AACHIE NYIMBO MPYA

Mwanamuziki wa Goodlife Crew, Weasel Manizo amewatolea uvivu mashabiki zake wanaomshinikiza kila mara kuachia nyimbo mpya.

Katika mkao na wanahabari Weasel amesema kwa sasa hataki kusikia mambo ya muziki na hana mpango kabisa  wa kwenda studio kurekodi nyimbo mpya kwani amejikita zaidi kwenye suala la kuiburudisha nafsi yake.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Bread & Butter” amesema pia hana mpango wa kuja na tamasha la muziki ambapo amewataka mashabiki zake wawasapoti wasanii ambao tayari wameshatangaza kufanya matamasha yao ndani ya mwaka huu.

Hata hivyo hajabainika nini hasa kimepelekea msanii huyo kuzungumza hayo ila wajuzi wa mambo nchini uganda wamedai kuwa weasel hajawahi rejea katika hali yake ya kawaida tangu msanii mwenzake Radio afariki mwaka wa 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *