
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Weasel Manizo ameweka wazi mpango wa kuja na tamasha la kila mwaka kwa ajili ya kumpa heshima marehemu Mozey Radio.
Msanii huyo ambaye alikuwa mwanakikundi wa Goodlyfe Entertainment, amesema tamasha hilo litaitwa Radio Festival na litaanza mapema mwaka wa 2022.
Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamemjia juu baada ya msanii huyo kususia kuhudhuria maombi ya kumkumbuka marehemu Radio wiki iliyopita wakimtaja kuwa mnafiki kwa kushindwa kuendeleza nyayo za mozey radio kwenye tasnia ya muziki nchiniΒ Uganda.
Duru za kuaminika zinasema Weasel Manizo alisusia maombi kutokana na tofauti walizonazo na Familia ya Mozey Radio kuhusu mirabaha ya muziki wa Radio.
Utakumbuka Mozey Radio ambaye alikuwa anaunda kundi la Goodlyfe alifariki mwezi Februari mwaka wa 2018 baada ya kuingia kwenye ugomvi na mlinzi wa night club moja huko Kampala uganda.