Entertainment

WEEZDOM AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANADADA CAROL LEEHAVI, ADAI UHUSIANO WAO ULIKUWA KIKI

WEEZDOM AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANADADA CAROL LEEHAVI, ADAI UHUSIANO WAO ULIKUWA KIKI

Msanii wa muziki nchini Weezdom amekiri kutumia kiki kutangaza wimbo uitwao Wazae aliyoshirikishwa na Carol Leehavi

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Weezdom amesema hata uhusiano wake wa kimapenzi na mrembo huyo ulikuwa batili na ilikuwa ni njia ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye tasnia ya muziki nchini kenya.

Msanii huyo ametangaza kurejea kwa kishindo kwenye muziki wake atakapoachia wimbo wake mpya  ambao  kwa mujibu wake hatatumia nguvu nyingi kuitangaza kwani ni moto wa kuotea mbali.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wametilia shaka tamko lake hilo ikizingatiwa kuwa amekuwa mtu wa mzaha sana kwenye muziki wake baada ya kuendekeza sana kiki badala ya kuachia muziki mzuri.

Kauli ya Weezdom imekuja siku chache baada ya uhusiaano wake Carol Leehevi kuingiwa na ukungu baada ya wawili hao kurushiana maneno makali mtandaoni, jambo lilomfanya mwanamuziki huyo kurudiana na ex wake wa zamani Mylee Stacy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *