Entertainment

Wema Sepetu Awajibu Wakosoaji wa Mavazi Yake kwa Kauli ya Kejeli

Wema Sepetu Awajibu Wakosoaji wa Mavazi Yake kwa Kauli ya Kejeli

Msanii nyota wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu, ametoa kauli yenye kejeli kufuatia wimbi la ukosoaji aliopewa mtandaoni kuhusu mavazi aliyovaa katika hafla ya hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameonekana kuchoshwa na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa baadhi ya mashabiki na wafuasi wake, akiamua kuwatolea majibu kwa maneno yenye utani mzito.

Katika ujumbe huo ulioandikwa kwa mtindo wa kuchekesha lakini wenye ujumbe mzito, Wema alisema:

“Next time navaa Baibui kubwa sana na Ninja… Gloves na Socks nyeusi na Miwani… Msijali wapendwa…”

Ujumbe huo umetafsiriwa kama majibu ya wazi kwa wale waliomkosoa kwa madai ya kuvaa mavazi yasiyoendana na maadili au mila za Kitanzania, hasa kwenye maeneo ya hadhara. Wema ameonesha dhahiri kuwa hakubaliani na mtazamo huo, na badala yake, ameonesha kuwa atendelea kujiamini na kuwa huru katika uchaguzi wa mavazi yake.

Baada ya kauli hiyo, mjadala umeendelea kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii huku mashabiki wakigawanyika. Baadhi wameunga mkono msimamo wa Wema, wakisema kuwa ana haki ya kuvaa anavyotaka, ilimradi hafanyi kosa la kisheria. Wengine, hata hivyo, walisisitiza kuwa kama mtu maarufu, anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa, hasa kwa vijana wa kike.

Sio mara ya kwanza kwa Wema Sepetu kujikuta kwenye vichwa vya habari kutokana na mavazi yake. Mara kadhaa amekuwa akikosolewa vikali, lakini pia amekuwa akipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wake waaminifu. Wema, ambaye ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 2006 na muigizaji aliyeshiriki katika filamu nyingi, amekuwa kwenye macho ya umma kwa zaidi ya muongo mmoja, hali ambayo imekuwa ikimuweka kwenye darubini ya mitazamo mbalimbali ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *