WhatsApp imeanza kufanya majaribio ya kipengele kipya kitakachowezesha wanachama wapya wa group kuona historia ya mazungumzo ya masaa 24 yaliyopita mara tu wanapojiunga.
Hatua hii inalenga kuboresha uelewa wa mazungumzo na kuondoa utata unaotokea pale mtu anapoingia kwenye group bila kufahamu kilichokuwa kinaendelea.
Kipengele hiki kikizinduliwa rasmi, kitawapa urahisi wanachama wapya kufuatilia mijadala ya karibuni, badala ya kutegemea ufafanuzi kutoka kwa wengine. Uboreshaji huu unatarajiwa kuleta mtiririko mzuri wa mawasiliano ndani ya groups, hasa zile zenye shughuli nyingi na mijadala inayoendelea muda mwingi.
Kwa sasa, WhatsApp inaendelea kukifanyia majaribio kabla ya kutangazwa kwa upana kwa watumiaji wote.