Tech news

WHATSAPP MBIONI KUWEKA MFUMO WA REACTIONS KATIKA CHATS ZA WATUMIAJI WAKE

WHATSAPP MBIONI KUWEKA MFUMO WA REACTIONS KATIKA CHATS ZA WATUMIAJI WAKE

Kwa muda mrefu WhatsApp imeendelea kufanya majaribio ya kuweka mfumo wa Reactions katika chats.

Reactions ni mfumo wa kuonyesha hisia au response yako katika message, unaweza kuonyesha kupendezwa, kushangaa, kucheka au kupinga jambo kwa kuchagua emoji inayoendana na mtazamo wako.

Feature hii ipo katika Facebook na Instagram lakini katika platform hizo unaweza kuchagua emoji yoyote.

Hivi karibuni WhatsApp imekuwa ikijaribu mfumo wa reactions katika app yake ya PC. Imeanza na app ya Mac na soon itaanza majaribio kwa watumiaji wa Windows.

Inaonekana WhatsApp inakamilisha majaribio katika platform zote kabla ya kuachia mabadiliko hayo kwa watumiaji wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *