Tech news

WhatsApp Yaanza Majaribio ya Kutaja Wajumbe Wote wa Kundi kwa Pamoja

WhatsApp Yaanza Majaribio ya Kutaja Wajumbe Wote wa Kundi kwa Pamoja

Kampuni ya WhatsApp imeanza kufanya majaribio ya kipengele kipya kinachowawezesha watumiaji kutaja wajumbe wote wa kundi kwa mara moja, badala ya kutumia alama ya @ kwa kila jina mmoja baada ya jingine.

Kupitia kipengele hicho, kila mshiriki wa kundi atapokea taarifa (notification) inayoonyesha kuwa ametajwa kwenye ujumbe fulani. Hatua hii inalenga kuongeza ufanisi wa mawasiliano hasa kwenye makundi ya kazi, familia, na miradi ya kikazi ambapo ujumbe muhimu unahitaji kuwafikia watu wote kwa haraka.

Kipengele hicho kipya kinatarajiwa kusaidia sana watumiaji wanaoshirikiana kwenye miradi au mijadala mikubwa, kwani kitapunguza muda wa kuandika na kuhakikisha kila mshiriki anapokea ujumbe muhimu.

Wataalamu wa masuala ya teknolojia wanasema kuwa hatua hii ni ishara kwamba WhatsApp inaendelea kuimarisha huduma zake kuelekea mfumo wa community-style interaction, sawa na ule unaotumika kwenye majukwaa kama Telegram na Discord.

Kwa sasa, kipengele hicho kipo katika hatua za majaribio, na kitarajiwa kuzinduliwa rasmi baada ya majaribio kukamilika na kupata mrejesho mzuri kutoka kwa watumiaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *