Tech news

WhatsApp Yazindua Kipengele Kipya cha “Save as Draft” kwa Status

WhatsApp Yazindua Kipengele Kipya cha “Save as Draft” kwa Status

Mtandao wa mawasiliano ya simu, WhatsApp, unakaribia kuongeza kipengele kipya kitakachowarahisishia watumiaji wake kuandaa na kuhifadhi Status kabla ya kuzipost. Kipengele hicho kipya, kinachoitwa “Save as Draft”, kwa sasa kinapitia hatua za majaribio (beta testing).

Kupitia mabadiliko haya, watumiaji wataweza kuhifadhi Status wanayoitengeneza endapo wataondoka kwenye ukurasa wa kutengeneza bila kupost. Hii ina maana kwamba hutalazimika kuanza upya kila unapokatishwa na shughuli nyingine kwenye simu.

Mara utakapofungua tena sehemu ya Status, utaona eneo maalumu la Drafts litakalokuwa na Status zote ulizohifadhi kwa muda bila kuzichapisha. Kutoka hapo, mtumiaji ataweza kuendelea kuhariri, kubadilisha au kupost bila kupoteza chochote.

WhatsApp inatarajia kuweka kipengele hiki kwa watumiaji wote mwishoni mwa mwaka huu, mara baada ya kukamilisha majaribio na kuhakikisha kinafanya kazi kwa usahihi katika vifaa vyote.

Kipengele cha “Save as Draft” kinatarajiwa kuongeza urahisi, muda, na ubora katika uundaji wa Status, hasa kwa watumiaji wanaokatishwa mara kwa mara au wanaopenda kurekebisha maudhui kabla ya kuyatangaza kwa marafiki na familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *