
Mwanamuziki na mwiigizaji kutoka Marekani Will Smith amemuomba radhi mchekeshaji Chris Rock pamoja na watayarishaji wa Tuzo za Oscars kufuatia tukio la kumchapa kofi mchekeshaji huyo live Jukwaani wakati wa ugawaji wa Tuzo hizo za 94 usiku wa kuamkia Machi 28, katika ukumbi wa Dolby Theatre, Hollywood nchini Marekani.
Will Smith ambaye tayari aliomba radhi akiwa Jukwaani punde baada ya kitendo kile, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameomba radhi tena kwa kusema kitendo kile hakikubaliki kwa namna yoyote.
Mwiigizaji huyo amesema anapokea utani wa aina yoyote lakini utani juu ya mke wake Jada Pinkett na afya yake alishindwa kuuvumilia.
“Ningependa mbele ya Umma kukuomba radhi Chris Rock, nilikuwa nje ya mstari na nilikosea. Nimejifedhehesha, na vitendo vyangu havikuwa dira au mfano wa Mwanaume ambaye natakuwa kuwa. Hakuna nafasi ya vurugu kwenye hii dunia ya upendo na ukarimu. Pia naomba radhi kwa Academy na watayarishaji wa show, wahudhuriaji wote na watazamaji.” aliandika Will Smith na kumalizia kuwa anajutia kwa kitendo kile.
Aidha, imeripotiwa kwamba usimamizi wa tuzo za Oscar unaandaa mkutano wa dharura kuamua hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Will Smith