Entertainment

WILL SMITH APATA OFA NYINGI ZA KUIGIZA FILAMU MAREKANI

WILL SMITH APATA OFA NYINGI ZA KUIGIZA FILAMU MAREKANI

Mwigizaji kutoka nchini Marekani Will Smith ameripotiwa kupata ofa nyingi za kuigiza filamu mbalimbali licha ya kufungiwa miaka 10 kuhudhuria kwenye hafla yoyote ile ya Oscars.

Kwa mujibu wa Jarida la Daily Star, Smith amepata ofa nyingi za kuigiza na tayari makampuni mengi ya kustream filamu yanafanya jitihada za kufanya nae kazi tangu tukio lake la kumpiga kibao mchekeshaji Chris Rock wakiwa jukwaani kwenye hafla ya tuzo za Oscars.

Tukio hilo la Will Smith limeonekana kutoathiri kabisa kazi zake za filamu, licha ya wengi kudhania kwamba lingeweza kumnyima baadhi ya dili mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *