Entertainment

Willy Paul afunguka gharama aliyotumia kutayarisha wimbo wake mpya

Willy Paul afunguka gharama aliyotumia kutayarisha wimbo wake mpya

Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo Willy Paul ameweka wazi gharama aliyotumia kutayarisha wimbo wake mpya uitwao “Umeme”.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram bosi huyo wa Saldido amejinasibu kuwa alitumia kiasi cha shillingi laki 5 kurekodi audio ya wimbo huo huku kutayarisha video ikimgharimu takriban shilling million 2 za Kenya.

Haikushia hapo ameenda mbali zaidi na kujinadi kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kutumia kiasi hicho cha fedha katika tasnia ya muziki nchini Kenya.

Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa mwaka 2023 ataangazia ubora kwenye kutayarisha kazi zake za muziki na sio idadi ya nyimbo ambazo hazina ubora wowote.

Kauli ya Willy Paul inakuja wakati anajiandaa kuachia video ya wimbo wake mpya “Umeme”, ambayo audio yake imefikisha Zaidi ya views laki 3 kwenye mtandao wa Youtube tangu iachiwe rasmi mapema mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *