
Mionekano kwa wasanii si jambo la kuchukulia poa, bali ni kazi. Ni moja ya njia za branding na kujiweka machoni mwa mashabiki muda wote.
Msanii nyota nchini Willy Paul amefunguka sababu za kunyoa nywele zake aina ya dreadlocks wiki iliyopita.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Willy Paul amesema kuwa ameamua kuja na muonekano mpya kwa sababu ameacha kabisa miendo yake ya zamani ambayo amedai kuwa yalimletea matatizo kwenye safari yake ya muziki.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Chocolate” ameweka wazi sababu ya ukimya wake kwenye mitandao ya kijamii akisema kwamba kuna project ambayo anaifanyia kazi kwa sasa hivyo mashabiki wakae mkao wa kula.