Entertainment

WILLY PAUL AHIRISHA TENA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

WILLY PAUL AHIRISHA TENA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini Willy Paul ametangaza hataachia album yake mpya iitwayo “The African Experience” kama ilivyokuwa imepangwa.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Willy Paul amesema hatua ya kuahirisha kutoka kwa album hiyo ni fursa nzuri kwake kujiandaa vilivyo na kuwapa mashabiki wake kazi nzuri.

Hata hivyo, bosi huyo wa Saldido records hajasema album hiyo itatoka lini na ni mabadiliko yapi anayafanya.

African Experience album ambayo ilipaswa kutoka oktoba 22  ikiwa ni exclusive kwenye jukwaa la boomplay, ina jumla ya nyimbo 17, ikiwa na kolabo 5 pekee kutoka kwa wakali kama Juma Jux, Eddy Kenzo,Daphne,Fik Fameica na Kelly Khumalo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *