
Staa wa muziki nchini Willy Paul ameonesha kusikitishwa na kampuni ya safaricom kutoongeza mapato ya wasanii kupitia Skiza tune.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa instagram willy paul ameisuta vikali kampuni ya safaricom akitaka maelezo kamili kuhusu kupunguzwa kwa mapato ya wasanii kupitia skiza tune.
Himaker huyo wa ngoma ya toto amesema alitarajia mapato ya skiza tune ya wasanii itaongezeka baada ya rais Kenyatta kutia saini msaada wa hakimiliki kuwa sheria, mswaada ambao ungetoa fursa kwa wasanii kufaidi na mapato ya kazi zao.
Utakumbukwa sheria mpya ya hakimiliki ilipendekeza wasanii kupata asilimia 52 ya mapato yao kupitia kazi zao huku huku mtoa huduma wa mawasiliano akiambulia asilimia 43 Â ya mapato.