Entertainment

Willy Paul Akanusha Madai kuwa VJ Patelo Ndio Amefanya Wimbo Wake Kuwa Hit

Willy Paul Akanusha Madai kuwa VJ Patelo Ndio Amefanya Wimbo Wake Kuwa Hit

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Willy Paul, amekanusha vikali madai yanayosambaa mtandaoni kwamba umaarufu wa wimbo wake mpya “Hii Design” umetokana zaidi na dance challenge ya VJ Patelo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Willy Paul amepinga vikali madai hayo, akisema kuwa mafanikio ya wimbo huo yanatokana na ubora wake, sio juhudi za mtu mmoja kama inavyodaiwa.

Amesema kuwa watu wanapaswa kuacha kudharau kazi yake na kuhusisha mafanikio ya “Hii Design” na challenge hiyo pekee, akisisitiza kuwa wimbo tayari ulikuwa na nguvu kubwa wenyewe.

Msanii huyo ameongeza kuwa track hiyo ni kali na imepokelewa vyema na mashabiki hata kabla ya challenge kuanza kusambaa.

Tangu kuachiwa kwa wimbo huo, baadhi ya mashabiki wamekuwa wakidai kuwa challenge ya VJ Patelo imechangia pakubwa kupandisha watazamaji na kuifanya ngoma hiyo kuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *