Entertainment

WILLY PAUL AKANUSHA TAARIFA ZA KUIUA CAREER YA MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA DIAMOND PLATINUMZ

WILLY PAUL AKANUSHA TAARIFA ZA KUIUA CAREER YA MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA DIAMOND PLATINUMZ

Baada ya Kurasa moja ya udaku nchini kwenye mtandao wa Instagram kuchapisha taarifa kuwa Willy Paul ana mpango wa kuimaliza career ya msanii wa Bongofleva Diamond Platinumz tarehe 17 mwezi Aprili mwaka huu, msanii huyo ameibuka na kukanusha taarifa hizo.

Kupitia uwanja wa comment ya post hiyo Willy Paul amesema madai hayo hayana msingi wowote kwani post yake ilitafsiriwa vibaya.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Toto” amesema post yake kwenye mtandao wa instagram ililenga kutangaza jambo lake ambalo litafanyika April 17 mwaka huu ingawa hakuweka wazi kama ni project ya wimbo au show.

Utakumbuka Willy Paul kupitia Instagram Page yake aliandika ujumbe unaosomeka “Nimetangaza rasmi vita. Nizuie kama una uwezo, Aprili 17 nitazika mtu. Mimi sio Simba. Jina langu ni Willy Paul almaarufu Black Panther.”

Ujumbe huo ulitafsiriwa moja kwa moja kumlenga Diamond platinumz ambaye amekuwa akijiita Simba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *